Klabu ya Shangai Shenhua inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Gus Poyet imepata ushindi wa 1-0 katika mchezo wa fainali ya kwanza wa kombe la ligi ya China dhidi ya Shangai SIPG.
Alikuwa ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Newcastle na timu ya taifa ya Nigeria, Obafemi Martins aliyetumia dakika 11 tu kuifanya klabu yake itoke na ushindi huo wa michezo ya fainali.
Obafemi Martins mwenye miaka 33 alitumia pasi nzuri na kupasia nyavu kiulaini na kuifanya klabu yake kuwa na matokeo chanya kuelekea mchezo wa fainali ya pili ambapo Shangai Shenhua itakuwa nyumbani.
Post a Comment
Post a Comment