Kocha wa zamani wa klabu ya Man utd ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya West Ham united, David Moyes ameanza vibaya katika kampeni yake ya kuipokea klabu hiyo iliyokuwa chini ya kocha Slaven Bilic aliyetimuliwa kutokana na timu kufanya vibaya.
Alianza Hughes, kiungo wa Watford katika dakika ya 11 wa mchezo na kumfanya kocha Moyes apatwe na kizunguzungu, na mpaka mpira unaenda mapumziko Watford 1-0 West Ham.
Kipindi cha pili dakika ya 64, kinda wa kibrazil, Richarlison akaifungia tena Watford goli la pili na kuifanya klabu kukamilisha mahesabu mapemaa kabla mpira haujaisha.
Kwa matokeo haya yanaifanya West Ham kuwa na wakati mgumu ikifurukuta kujitetea katika nafasi za kushuka daraja.
Post a Comment
Post a Comment