Kocha Gian Piero Ventura ametimuliwa rasmi katika timu ya taifa ya Italia mara baada ya kushindwa kuisaidia timu hiyo kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani uko nchini Urusi.
Ventura alishindwa kuiwezesha timu hiyo kufuzu kucheza kombe la dunia mara baada ya kupoteza kwa magoli ya jumla ya 1-0 na kuifanya Italia kutokufuzu kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka mwaka 1958.
Mara ya mwisho kwa kocha huyo kuongea juu ya hatima yake alisema "kikubwa ni kuomba msamaha kwa waitalia kwa kilichotokea, ingawa tulikuwa na uwezo wa kushinda na kufanikiwa kufuzu".
Post a Comment
Post a Comment