Klabu ya Chelsea imepeleka tena maombi ya kumsajili nyota wa Gabon, Pierre Aubameyang ambaye anaichezea klabu ya Borussia Dortmund.
Inaelezwa nyota huyo amekuwa hana uhusiano mzuri na klabu yake ya sasa kutokana na mfululizo wa matukio yake ambayo yamemfanya kupewa adhabu mara kwa mara.
Aubameyang alishawai kuachwa na kikosi chake hicho mara baada ya kusafiri kwenda Italia bila ridhaa ya klabu na msimu huu alishawai kuachwa tena nje kutokana na utovu wake wa nidhamu kabla ya kushuhudiwa pia akipewa kadi nyekundu katika mchezo wa ligi kuu wikiendi iliyopita ambapo klabu yake ilikuwa inaongoza 4-0 kabla ya Schalke kurudi kipindi cha pili na kuchomoa magoli yote na mchezo kuisha kwa sare ya 4-4.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anamtaka nyota huyo ambapo dirisha la usajili likiwa limebakiza mwezi mmoja kabla ya kufunguliwa.
Post a Comment
Post a Comment