Baada ya suluhu ya mchezo wa klabu ya Schalke 04 ilioupata katika mchezo dhidi ya Borrusia Dortmund ambapo Schalke ilitoka nyuma kwa magoli 4-0 mpaka kutoa suluhu ya magoli 4-4 inaelezwa kuna mpango kabambe umepanga na klabu ya Schalke 04 ili kumzuia nyota wake asiondoke.
Leon Goretzka ndiye nyota anayeiumiza kichwa kwa sasa klabu hiyo mara baada ya kuhusishwa na kutakiwa na klabu kubwa ambazo ni Real Madrid, Barcelona na Juventus.
Sasa ili kumzuia nyota huyo ili asishawishike kuondoka klabuni hapo, moja ya viongozi wa klabu hiyo alisema "tunaamini ushindani ule ulioonyeshwa kwenye mechi dhidi ya Borrusia basi tunaamini ulimvutia Leon (Goretzka) na inaweza kumfanya aghaili kuondoka hapa"
Goretzka aliingia akitokea benchi wakati huo matokeo yalikuwa ni 4-0 tayari Schalke kashafungwa, lakini kuingia kwake ni kama kuliiamsha timu na kufanikiwa kuchomoa magoli hayo na kutoka suluhu.
Mkataba wa Goretzka klabuni hapo unaisha mwezi juni mwaka 2018 ambapo mpaka sasa kuna mazungumzo yanaendelea kufanyika ili nyota huyo asaini mkataba mpya utakaomfanya apokee mshahara wa euro milioni 12 ambapo kama akisaini mkataba huo timu ikitaka kumsajili itabidi ilipe kiasi cha euro milioni 50.
Post a Comment
Post a Comment