Mchezo wa Basseball hauna mashabiki wengi nchini Tanzania, na haujafahamika sana katika nchi za Afrika Mashariki ingawa kuna nchi zinatengeneza ajira na vipaji vingi kupitia mchezo huu ambao unaelezwa kujichimbia sana katika nchi za bara la Asia, haswa nchini Japan.
Nchini Tanzania kulianzishwa kampeni ya kuanzisha mchezo huu ambao unafananishwa sana na mchezo wa Cricket ambapo kwa Dar es Salaam, wakufunzi kutoka nchini Japan walifika na kuanzisha akademi katika shule za Azania sekondari na shule ya Benjamin William Mkapa.
Sasa kuelekea mwisho wa mwaka huu kutakuwa na mashindano ya kitaifa ya mchezo huo ambapo timu mbalimbali kutoka Tanzania mikoa ya Dar, Zanzibar, Sanya Juu, Iringa, Dodoma na Mbeya zitashiriki mashindano hayo ambayo pia kutafanyika uchaguzi wa kuchaguliwa wachezaji watakaounda timu ya taifa ya mchezo huo kujiandaa na mashindano ya Afrika Mashariki yaliyokuwa yanategemewa kufanyika nchini Kenya kabla ya kughairishwa na kupangwa kufanyika mkoani Mwanza.
Mashindano ya kitaifa ambayo yatatumika kuchagua wachezaji hao yatafanyika mkoani Dar es Salaam katika shule ya Azania siku ya ijumaa ya mwezi desemba tarehe 1 ambapo yatafanyika kwa siku tatu na kumalizika tarehe 3 ya mwezi desemba.
Nadhani ni wakati mwafaka kwa wananchi na serikali na taasisi nyengine kuangalia nje ya soka ili kutengeneza vipaji vingi kupitia michezo mbalimbali.
Je unataka kuviona vipaji vya vijana wa kitanzania katika mchezo huu? tukutane tarehe 1 mwezi desemba pale Azania sekondari.

Post a Comment
Post a Comment