Klabu ya Barcelona ya nchini Hispani imepanga kufanya usajili wa kuwashangaza wengi katika dirisha hili la usajili linalokuja.
Barcelona mara baada ya kumuuza nyota wake Neymar kujiunga na klabu ya PSG kwa dau lililovunja rekodi ya dunia, kiasi cha paundi 198 na ikamsajili nyota kutoka Borrusia Dortmund na raia wa Ufaransa, Moussa Dembele ingawa nyota huyo ametumia muda mwingi akiwa kama majeruhi. Sasa Barcelona imepania kushtua wengi mara baada ya habari kuenea kwamba klabu hiyo imefikia hatua za mwisho katika kumsajili nyota mwengine kutoka Ufaransa anayeichezea klabu ya Atletico de Madrid, Antoinne Griezmann.
Inaelezwa kwamba makubaliano baina ya pande hizo mbili yaani uongozi wa klabu ya Barcelona na Atletico umefikia hatua za mwishoni kukamilisha dili hilo.
Huku mwenyewe Griezmann akielezwa kwamba atafurahi ikiwa siku moja atakuja kucheza timu moja na Lionel Messi, Luis Suarez na Andres Iniesta.
Dau la Griezman linatajwa kufikia paundi milioni 170.
Post a Comment
Post a Comment