Klabu ya Barcelona inadaiwa imejitoa kwenye mbio za kumsajili nyota raia wa Ujerumani, Mesut Ozil.
Inaelezwa klabu hiyo ilikuwa ikimfukuzia nyota huyo anayeichezea klabu ya Arsenal kama mbadala endapo ikimkosa kiungo wa Liverpool, Phillip Coutinho ingawa sasa inaonekana kujitoa kwenye mbio hizo za kumuwania raia huyo mjerumani ambaye alishawai kuichezea Real Madrid ya Hispania.
Ambapo moja ya sababu inayoelezwa ya Barcelona kuachana na mjerumani huyo ni mara baada ya kiungo huyo kudai mshahara wa paundi 330,000 mshahara ambao klabu ya Barca inauona ni mkubwa sana kwa kiungo huyo.
Post a Comment
Post a Comment