Magaidi 6 wa al shabaab mikononi mwa polisi nchini kenya baada ya kukamatwa wakijaribu kufanya shambulzi la kigaidi

Inspekta Mkuu wa Polisi nchini humo Joseph Boinnet amesema washukiwa hao, wawili raia wa Kenya na wengine kutoka Somalia, walikuwa wametumwa na Kamanda wao kutoka kambi yao ya Burhanche.
Boinett amesema, maafisa wa usalama nchini Kenya walifanikiwa kuzuia shambulizi hilo kwa sababu ya ushirikiano wa karibu na wenzao wa Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mafanikio haya ya jeshi la Polisi nchini humo limekuja baada ya maafisa 20 wa Polisi kuuawa wiki kadhaa zilizopita Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya magari waliyokuwa wanasafiria kukanyaga mabomu yaliyotegwa ardhini.
Kenya imeendelea kutishiwa usalama na kundi la Al Shabab baada ya kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na kundi hilo mwaka 2011.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.