Mzozo wa kisiasa unaendelea kushuhudiwa nchini Gabon, wiki moja kamili tangu kufanyika kwa uchaguzi wa urais nchini humo na rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wiki hii.
Watu watano wameuawa na maelfu kukamatwa katika makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na jeshi la polisi jijini Libreville.
Aliyekuwa mgombea wa upinzani Jean Ping amejitangaza rais wa nchi hiyo na kudai kuwa yeye ndiye aliyeshinda.
Hatua hii inatarajiwa kuzua mgogoro zaidi wa kisiasa nchini humo katika siku zijazo.
Ping ambaye alikuwa amezuiliwa katika Makao makuu ya chama chake amesisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda na kueleza kuwa dunia inajua hilo.
"Kila mmoja duniani anafahamu nani ndio rais wa Jamhuri, ni mimi," amesema Ping.
Aidha, ametaka kura kuhesabiwa upya ili kubaini ukweli wa mambo kuhusu mshindi wa uchaguzi huo na kuitaka pia Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati mzozo huo haraka iwezekanavyo ili kumaliza machafuko yanayoshuhudiwa.
Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake kuhusu kinachoendelea nchini humo na kutaka uvumilivu kutoka pande zote mbili na kusikitishwa kwa machafuko.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.