kiasi cha kuwafanya watu waamini muziki huo siyo uhuni bali ni kazi.
Mwana FA kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV alisema Professor Jay pamoja na marehemu Albert Mangwea ndiyo wasanii wake wawili bora wa siku zote katika muziki wa Hip hop Tanzania.

Mbali na hilo Mwana FA alisema kuwa Professor Jay ni msanii ambaye alifanya yeye kidogo aache muziki sababu Mwana FA alikuwa anataka kufanya muziki bora lakini alipokuwa anasikiliza kazi za Professor Jay akaona hawezi kufanya kazi bora kama hizo.
"Unajua mimi siku zote huwa nataka kuwa best kwa kile nachofanya sijui kwa wasanii wengine, sasa baada ya kusikia ngoma ya Professor Jay 'Chemsha bongo' mimi nina nyimbo zangu nilikuwa nimeandika nikarudi nyuma nakajiuliza sasa mimi nawezaje kuwa 'best' kwa ngoma hizi? Yaani alinikatisha tamaa lakini nikarudi na kuanza kujipanga upya" alisema Mwana FA
Post a Comment
Post a Comment