Jeshi la polisi mkoanj mbeya linawashikilia raia wawili wanaodaiwa kusambaza habari mtandaoni ambazo zinaeza hatarisha amani ya nchi.
Hatua hiyo pia inayohusishwa na Tukio la Oparesheni Ukuta lililopangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) lifanyike Septemba mosi mwaka huu licha ya serikali kupinga jambo hilo.

Kamanda Kidavashari ameonya wafuasi wa Chadema na wananchi wengine kuepuka kusambaza jumbe zinazoonekana kukiuka miiko na maadili ya Utaifa na pale wanapotumiwa kabla ya kuzituma kwa watu wengine wazifute au kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.
Amewataka pia wananchi kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa na mamlaka huku akisisitiza kuwa hata maandiko matakatibu katika baadhi ya vitabu vya dini yanaeleza kuwa Kila Mamlaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu.
Post a Comment
Post a Comment