MKAZI wa kijiji cha Busongo, kata ya Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Monica Manyabhuluba, ameuliwa na mumewe kwa kupigwa na nyundo kichwani, baada ya kuibuka ugomvi wa kimapenzi kutokana na mwanamume huyo kupigiwa simu na mwanamke mwingine.
Akithibitisha tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, alimtaja mwanamume anayetuhumiwa kutenda mauaji hayo kuwa ni Deus Shitungulu, mkazi wa kijiji hicho, aliyetenda kosa hilo saa 5:00 usiku na kukimbia.
Alisema Polisi inaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma inayomkabili.
Aidha, aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake watumie vyombo vya usuluhishi kumaliza migogoro.
“Chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kati ya mume na mke. Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa kwakuwa alikimbia baada ya tukio,” alisema.

Post a Comment
Post a Comment