Msanii Malaika amezidi kuwaweka watu mbali mbali kwenye kigugumizi juu ya tetesi za yeye ni mshirika wa dini ya kishetani, wajenzi au free mason
Malaika ambaye wachunguzi wa mambo wamesema anapenda kutumia namba inayohushwa na imani hiyo ya kishetani ya 666, ambayo hata namba yake ya simu inaishia 666, amesema hatolizungumzia suala hilo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema muda muafaka utakapofika ataweka wazi kila kitu.
“Sitopenda kuizungumzia ila niseme tu kwamba ni namba ambayo naipenda, nimepata simu nyingi sana, interviews lakini siku nitakayoamua kuongelea nitaongea kuhusu hivyo, lakini kwa sasa hivi siko tayari”, alisema Malaika.
Pia Malaika amesema hata jina lake la Malaika ambalo watu wanamtuhumu haendani nalo kutokana na mambo hayo, amesema hajali kuhusu hilo kwani hilo ni jina tu kama jina lingine.
Kwenye akaunti yake ya instagram, Malaika ameandika wasifu wenye kushtua watu, ambao amehusisha na Illuminati ndani yake.

Post a Comment

HABARIKA said... 2 July 2016 at 07:53

Hana lolote anatafuta kiki tu.Wakina Jay Z wanazungumza hadharani na kila mtu anajua hawafichi fichi.
Tukiachana na hilo, huyu dada ni mrembo kwel kwel

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.