Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili nchini asubuhi ya leo na kupokewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Baada ya kuwasili na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Rwanda amepokea heshima za kijeshi pamoja na kukagua gwaride na kutizama vikundi mbalimbali vya ngoma na tarumbeta vilivyoandaliwa kwa ajili yake.


Ziara ya Rais Kagame imefuatia mwaliko wa Rais Dkt. John Magufuli ambapo atakuwepo nchini kwa siku mbili ambapo baada ya kuwasili amefanya mazungumzo na mwenyeji wake na baada ya hapo atazungumza na wanahabari na usiku atashiriki dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Dkt. John Magufuli.

Lengo la Rais Kagame kuja nchini ni kuzindua maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Sababasa ambayo inazinduliwa leo ili wafanyabishara na wajasiriamali kuweza kuonyesha na kuuza bidhaa ambazo wanazalisha katika maeneo mbalimbali.
Aidha biashara ya kimataifa ya sabasaba husaidia watu kutoka mataifa mbalimbali kuweza kujumuika na watanzania katika kuonyesha namn kampuni taasisi au biashara zao wanavyoziendesha na kutoa huduma kwa wananchi.

Ziara ya Rais Kagame pia inaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda ambapo mwezi April Rais Dkt. Magufuli aliitembelea Rwanda na kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.