Mara baada ya kocha wa Manchester city, Pep Guardiola kuchaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi Novemba, nyota wa Liverpool raia wa Misri, Mohammed Salah nae amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba.
Salah ameshinda tunzo hiyo muda mfupi mara baada ya kuchaguliwa pia kuwa mchezaji bora kutoka Afrika akichaguliwa na chombo cha habari cha BBC.
Mohammed Salah ambaye ni kinara katika ufungaji katika ligi kuu Uingereza amekabidhiwa zawadi yake hiyo ambapo mwezi Oktoba nyota wa Manchester city, Leroy Sane ndiye aliyeshinda tunzo hiyo.
Hongera simba wa Farao, Mohammed Salah
Post a Comment
Post a Comment