Timu ya taifa ya Hispania huenda ikatolewa katika ushiriki wa kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika huko nchini Urusi kutokana na siasa nchini humo kuonekana kuliingilia chama cha soka cha nchini humo maarufu kama RFEF.
Kumekuwa na mgogoro nchini Hispania ambapo kitongoji cha Catalunya ambacho ndicho kitongoji mwenyeji wa klabu za Barcelona na Espanyol kimekuwa kikizitumia timu hizo kama utambulisho wao kama nchi inayogombani uhuru lakini pia nchini Hispania kunategemewa kufanyika uchaguzi mkuu ambapo siasa inaonekana kuzihusisha sana klabu za michezo na chama cha soka nchini humo ambapo kwa katiba na sheria za FIFA hiyo sio haki. Ambapo sheria ya shirikisho hilo la FIFA inaagiza nchi wanachama wa shirikisho hilo inatakiwa ziwe na vyama huru vya soka.
Mnamo mwaka 2008, FIFA tayari iliwai kuitahadharisha Hispania kwa kutolewa kwenye mashindano ya Euro, ambapo hatimaye ilikuwa mabingwa, kutokana na mapambano kati ya Jaime Lissavetzky na Ángel María Villa.
Aliyekuwa rais wa FIFA kipindi hicho Sepp Blatter akiwa anaitahadhariwa Hispania alisema "Kamati ya dharura ya FIFA inaweza kukutana katika masaa sita na kuisimamisha Hispania, lakini hatutotaka hilo litokee"
Post a Comment
Post a Comment