Kocha wa Manchester united, Jose Mourinho ambaye ni raia wa Ureno alipofanya mkutano na waandishi wa habari na kuulizwa kuhusu mustakabali wa nyota wa klabu hiyo, Henrikh Mkhitaryan kuhusu nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza alisema "mi nachojua kwenye timu yangu kila mchezaji ana bei yake" akimaanisha kama kuna klabu inamtaka basi anaweza akauzwa.
Sasa hapa nakuletea nyota wa klabu hiyo ambao wanaweza kuondoka klabuni hapo muda wowote kuanzia sasa;
Henriky Mkhitaryan
Nyota huyo aliyesajiliwa na Mourinho pindi akiwa anafika klabuni hapo akitokea Borrusia Dortmund kwa dau la paundi milioni 30 anaonekana kutokuaminika tena na kocha Mourinho mara baada ya kufululiza kutokuanza katika michezo mitano msimu huu uku akiachwa kabisa bila kuitwa kwenye kikosi katika michezo takribani minne anaonekana hatakiwi tena klabuni hapo ukilinganisha pia na kauli aliyoitoa Mourinho kwa kusema kila mchezaji ana bei yake.

Marouane Fellaini
Raia wa Ubelgiji aliyetokea Everton kabla ya kusajiliwa na Man utd akivutwa na David Moyes aliyekabidhiwa kuiongoza Man utd wote wakitokea Everton anaonekana kutoendelea kuwepo tena kikosini hapo mara baada ya kutokufanyika mazungumzo yoyote ili kuongeza mkataba wa nyota huyo ambaye mkataba wake wa sasa na Man utd unaisha mwisho wa msimu huu. Je ataendelea kubaki? hakuna anayejua ingawa haonekani kuendelea kubaki.

Luke Shaw
Huyu ni mlinzi wa pembeni ambae ni raia wa Uingereza ambaye alipata majanga makubwa akitokea kwenye majeruhi na sasa amerejea kupambania namba klabuni hapo ingawa inaonekana ni ngumu kwake kutokana na kutokuaminika sana na kocha licha ya kurudi akiwa na hali nzuri akicheza michezo kadhaa na kufanikiwa kuwa ata nyota wa mchezo.

Post a Comment
Post a Comment