Chelsea bado haijawa sawa ikiwa imeshapoteza michezo minne mpaka sasa kwenye ligi kuu Uingereza huku ikishika nafasi ya tatu huku ikiwa imeachwa alama tatu na Man utd inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo leo itashuka darajani kumenyana na Huddersfield, Chelsea ikiwa ugenini. Mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa saa 23:00.

Kuelekea katika mchezo huo, Chelsea itaendelea kmkosa nyota wake David Luiz ambaye anasumbuliwa na majeraha huku Michy Batshuayi akionekana kuwa tayari kucheza mara baada ya kutoka kwenye majeruhi.

Lakinim kwa upande wa Huddersfield wao wapo kwenye hali ya ushindi kutokana na kushinda mchezo wao dhidi ya Brighton kwa magoli 2-1 lakini mpia wakiwa na faida ya kuwa nyumbani hali inayowza kuwafanya wapambane zaidi kutokana na kujua kuwa Chelsea haipo kwenye hali ya ushindio mara baada ya kupoteza ugenini katika mchezo dhidi ya west Ham kwa goli 1-0 jumamosi iliyopita.

Chelsea itashuka katika mchezo huu ikiwa na nia ya kushinda mchezo huu ili iweze kupunguza pengo dhidi ya Man utd inayoshika nafasi ya pili ikiwa imeachwa kwa alama 3 na wababe hao wa Manchester wakati kwa upande wa Huddersfield itashuka katika mchezo huu ikiwa nyumbani ikiwa nafasi ya 12 ikiwa na alama swa na Southampton inayoshika nafasi ya 11 na Huddersfield itataka kushinda mchezo huu iili ipande kutoka nafasi hiyo mpaka nafasi ya 10 inayoshikwa na Everton wenye alama 19.

Michezo mingine leo EPL;
Burnley vs Stoke city (saa 22:45)
Crystal Palace vs Watford (saa 23:00)

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.