Timu ya taifa ya Senegal imefanikiwa kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani uko nchini Urusi mara baada ya kuifunga Bafana Bafana kwa mabao mawili kwa nunge.

Haikuwa kazi ngumu sana kwa Senegal iliyo na nyota kadhaa akiwemo mshambuliaji mahiri wa klabu ya Liverpool, Sadio Mane ambapo katika dakika ya 13, Diafra Sakho akaipatia bao la kwanza Senegal na kuifanya iwe mbele na katika dakika 32, Thamanqa Mkhize wa Afrika Kusini akajifunga na kufanya mpaka mpira unaisha Senegal kushinda kwa mabao 2-0.

Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kufuzu toka ilipofanya hivyo mwaka 2002. Na inakuwa timu ya tatu kutoka Afrika kufuzu katika michuano hiyo mara baada ya Misri na Nigeria kufanya hivyo.

Hongereni Senegal.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.