Nyota na mchezaji ghali wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale amepata majeraha yatakayomfanya kukaa nje kwa muda mrefu.
Mchana wa leo klabu ya Real Madrid ilitoa taarifa kwamba mchezaji huyo amepata majeraha tena akiwa mazoezini kwenye mazoezi madogo madogo aliyokuwa anafanya mara baada ya kuwa chini ya uangalizi baada ya tarehe 26 mwezi septemba alipoumia katika mchezo dhidi ya Borrusia Dortmund na toka hapo hajawai kucheza tena mpaka hapo alipopata majeraha akiwa mazoezini katika msuli wa mguu wake wa kulia.
Majeraha hayo yanaweza kumfanya Bale kukaa nje zaidi licha pia ya kutokujiunga na timu yake ya taifa ya Wales akiendelea kujiuguza.
Post a Comment
Post a Comment