Baada ya kiwango kikubwa alichokionyesha katika msimu wake wa kwanza katika ligi kuu Uingereza, winga wa klabu ya Watford Richarlison sasa atakiwa na vigogo katika ligi kuu hiyo.
Chelsea na Tottenham zinatajwa kuwania saini ya nyota huyo raia wa Brazil mwenye miaka 20 ambapo uongozi wa klabu ya Watford umekataa kumuuza nyota huyo katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi januari.
Richarlison mpaka sasa ndiye mchezaji anayeongoza kuhusika katika magoli mengi ugenini ambapo kafunga magoli 4 na kutoa pasi za mwisho 3.
Post a Comment
Post a Comment