Ni siku nyengine tamu kwa mashabiki wa Man utd duniani kote mara baada ya kuishuhudia timu yao ikishinda mchezo mwengine dhidi ya Watford uwanjani Vicarage Stadium.

Alikuwa ni nyota Ashley Young aliyeipa ushindi muhimu kwa kufunga magoli mawili huku mengine yakifungwa na Antonio Martial na Jese Lingard waliofanya matokeo kuwa 4-2 dhidi ya Watford.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Man utd kupunguza lile pengo la alama lililokuwepo kati yake na Manchester city iliyopo kileleni kutoka alama 8 mpaka sasa kuwa alama 5.

Wakati hayo yakitokea kwa Man utd, huku Mauricio Pochettino akaishuhudia klabu yake ya Tottenham ikipoteza ugenini mara baada ya kupokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Leicester city kutoka katika uwanja wa King Power Stadium.

Ni Jamie Vardy na Riyad Mahrez walioipaisha klabu hiyo yenye jina la utani la "The Foxes" ikimaanisha Mbwa Mwitu ambapo inamfanya Pochettino kuwa na msimu mbaya ukilinganisha na aliyoyafanya msimu uliopita. Goli la Tottenham lilifungwa na Harry Kane.

Matokeo mengine EPL;
Brighton 0-0 Crystal Palace
West Brom 2-2 Newcastle

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.