Wakati jana ligi kuu Uingereza na Italia zikiendelea, huko nchinu Hispania kulikuwa na michezo ya kombe la Copa Del Ley ambapo Real Madrid ilikuwa inashuka uwanjani kumenyana na klabu ya Fuenlabrada ambapo Madrid ilikuwa nyumbani katika uwanja wake wa Santiago Bernabeu, na mchezo huo uliisha kwa sare ya 2-2, ambapo kwa matokeo ya jumla yakiwa ni 4-2 kutokana na Real kushinda mchezo wa kwanza.
Magoli yote ya Real Madrid yakifungwa na Mayoral wakati yale ya Fuenlabrada yakifungwa na Luis Mila na Portilla aliyefunga dakika ya 89.
Lakini wakati Madrid akifuzu katika michuano hiyo, huko Malaga akaangushwa na kutupwa nje katika michuano hiyo kwa kufungwa kwa magoli ya jumla ya 3-2 mara baada ya jana kutoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Numancia.
Matokeo mengine Copa del Ley;
Celta vigo 1-0 Eibar (jml; 3-1)
Levante 1-1 Girona (jml; 3-1)
Leganes 1-0 Valladolid (jml; 3-1)
Post a Comment
Post a Comment