"Mungu awafanyie wepesi,"
Hayo ndo yalikuwa maneno ya rais wa shirikisho la soka la Tanzania
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ametuma salamu za pole kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA), Athuman Kambi kufuatia ajali ya gari iliyopata timu ya Silabu ya Mtwara.
Gari iliyowabeba wachezaji wa Silabu – mabingwa wa Mkoa wa Mtwara ilipata ajali maeneo ya Mchinga mkoani Lindi wakiwa safarini kwenda Pwani kucheza na Kisarawe United katika mchezo wa awali wa kuwania Kombe la Shirikisho la Azam.
Hakuna aliyefariki lakini majeruhi ni 12 na wamelazwa hospitali ya mkoa wa lindi.
Post a Comment
Post a Comment