Ni wiki nyingine tena katika ligi ya mabingwa mchezo wa nne hatua ya makundi na tunakuketea uchambuzi na matokeo ya baadhi ya mechi kali za usiku wa jana.
TOTTENHAM 3-1 REAL MADRID
Baada ya kupata matokeo ya kushtusha katika ligi ya nyumbani dhidi ya wapanda daraja,Real madrid imezidi kukutana na mizimu msimu huu baada ya kupata kipigo kingine kikali kutoka kwa waingereza ambacho wengi hawakutegemea.
Kila timu inaweza kuwa na usiku mbaya kama jana Chelsea walivokufa kwa Roma 3-0 ,Lakini Madrid inaonekana kuwa na msimu mbaya.
Mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Klabu bingwa na mabingwa watetezi wa la liga,sasa wapo pointi tatu nyuma ya spurs kwenye makundi huku wakiwa pointi nane nyuma ya Barcelona katika ligi kuu ya uhispania.
Zidane anakazi kubwa ya kufanya kuhakikisha madrid inarudi kwenye ubora wake.
NAPOLI 2-4 MAN CITY
Kigogo mwingine wa kiingereza nae atoa dozi nzito akiwa ugenini mjini italia na kuweza kujihakikishia nafasi katika 16 bora ya ligi ya mabingwa msimu huu huku zikisalia mechi 2.
Mechi hiyo iliyokuwa ya aina yake huku mashabiki wa Napoli wakipiga kelele za kutosha kuona wanawachanganya Man city,lakini watoto hao wa Guardiola kadili muda na kelele zilivyozidi nao ndo walivyozidi kunawili uwanjani.
Man city ambao wapo kileleni kwa pointi 5 katika ligi kuu ya uingereza wanaonekana kuwa wanaweza wakawa tishio katika soka la ulaya kama wataendelea na mwendo huu.
Pia katika mechi hiyo straika Sergio aguero aliweka rekodi na kuwa mfungaji bora wa muda wote katika klabu ya man city.Rekodi hiyo iliyochukua miaka 11 kuiweka na miaka 78 kuitunza iliyikuwa ikishikiliwa na Eric Brook akiwa na magoli 177,imevunjwa jana usiku na aguero baada ya kufunga goli dhidi ya Napoli.
LIVERPOOL 3- 0 MARIBOR
Basi kubwa aina ya Tata"utani" walilopaki maribor anfield halikuweza kuwazuia Majogoo wa jiji kuziona nyavu zao mara tatu huku kiungo james milner akikosa penati kipindi cha pili.
Post a Comment
Post a Comment