Ligi kuu nyingi duniani zinatoa tunzo kwa waliofanya vizuri katika ligi hizo ambapo zinajumuisha wachezaji bora na makocha bora waliofanya vizuri kwa mwezi wa Oktoba.
Katika ligi kuu South Africa maarufu kama PSL zimetolewa tunzo mchana wa leo ambapo kwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba ameibuka kuwa Rodney Ramagalela ambaye ni mchezaji wa Polokwane City ambaye amefanya vizuri mwezi Oktoba mara baada ya kufunga katika kila mchezo kwa michezo 3.
Lakini pia kwa 5upande wa kocha bora wa mwezi Oktoba, tunzo hiyo imeenda kwa Veselin Julisic ambaye anaifundisha klabu ya Bloem Celtic.
Lakini pia tunzo ya goli bora la mwezi oktoba ilibebwa tena na yuleyule aliyeibuka mchezaji bora wa mwezi oktoba, Rodney Ramagalela.
Post a Comment
Post a Comment