Klabu inayomilikiwa na matajiri wa kiarabu nchini Ufaransa, PSG huenda ikalazimika kuwauza nyota wake wawili ili kwenda sawa na sheria za FIFA.
Klabu hiyo imepanga kuwauza Angel di Maria na Lucas Moura ambao wanaonekana kuwa na nafasi finyu kikosini hapo mara baada ya ujio wa nyota Neymar Jr aliyesajiliwa kwa dau la rekodi ya dunia akitokea Barcelona na Kylian Mbappe ambaye amesajiliwa akitokea AS Monaco.
Sheria ya FIFA inakataza kwa klabu kutumia kiasi kikubwa katika usajili bila kuuza na kumefanyika mkutano kati ya wawakilishi wa klabu hiyo na FIFA kuangalia uwezekano wa klabu hiyo kuweza kuepuka rungu la sheria hiyo na kuonekana inatakiwa klabu hiyo iuze nyota wake ili kuleta uwiano sawa kati ya kiasi kilichotumika kuuza na kununua wachezaji.
Post a Comment
Post a Comment