Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ambaye amesajiliwa akitokea Real Madrid katika dirisha kubwa la usajili la kipindi cha kiangazi amesema haamini kama mchezaji ghali duniani, Neymar Jr. anaweza kujiunga na Real Madrid.
"Madrid ni klabu kubwa, lakini siamini kama Neymar anaweza kujiunga na Madrid, ingawa hakuna linaloshindikana pale" alisema Morata ambaye aliwai kucheza Madrid katika vipindi viwili tofauti.
Neymar ambaye kwa sasa anaichezea PSG aliposajiliwa kwa dau lilivunja rekodi ya dunia ambapo alisajiliwa kwa kiasi cha paundi milioni 198 akitokea Barcelona klabu ambayo inapatakina ligi moja na klabu inayomfukuzia kwa sasa, Real Madrid ambapo huko anatakiwa ili akakabidhiwe ufalme wa Cristiano Ronaldo anayeonekana kutupwa na umri.
Post a Comment
Post a Comment