Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina ambaye ni nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi ameshindilia kwa msisitizo juu ya yeye kutohusika kuamuru mchezaji flani acheze na nani asicheze.
Messi alihojiwa juu ya je ni mshambuliaji gani wa kati anayepaswa kutumiwa na kocha wa timu hiyo, Jorge Sampaoli.
"hayo ni maamuzi ya kocha ambapo yeye ndiye wa kuamua kama namba tisa awepo Aguero, Higuain au Mauro Icardi" alisema Messi.
"mimi ni mchezaji kama wachezaji wengine sipaswi kuamua flani acheze na flani asicheze"
Messi amekuwa akishutumiwa kwamba yeye ndiye anasema flani na flani ndio wanastahili kuitwa kwenye kikosi cha Argentina, tuhuma ambazo alizikana.
Messi mchana wa leo ameiongoza timu yake ya taifa kutoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018, Urusi.
Goli hilo moja limefungwa na Kun Aguro.
Post a Comment
Post a Comment