Wakati ligi nyengine zikiendelea kutimua vumbi katika wiki nyengine ya muendelezo wa ligi kuu za barani Ulaya huko Hispania nako hali ni tete jioni na usiku wa leo.
Real Madrid watashuka dimbani kumenyana na Malaga ambapo mchezo huo utachezwa nyumbani Santiago Bernabeu mida ya saa 18:15.
Real Madrid imeanza kwa kusuasua ambapo nyota Cristiano Ronaldo anaonekana kupata tabu kwenda na kasi aliyokuwa nayo kabla. Lakini usiku huu atakuwa na nafasi nyengine ya kuidhihirishia dunia kwamba bado ana kitu kikubwa miguuni mwake na sio kwamba kaishiwa huku akifanya makubwa katika ligi ya mabingwa ulaya maarufu kama Uefa.
Michezo mingine katika La Liga;
Levante vs Atletico Madrid (saa 22:45)
Real Betis vs Girona (saa 20:30)
Mchezo ulioisha;
Alaves 1 vs 2 Eibar
Post a Comment
Post a Comment