Mshambuliaji na nyota wa klabu ya Liverpool, Mohammed Salah ameifungia klabu yake hiyo goli la kuongoza katika mchezo wa ligi kuu raundi ya 13 huku Willian akichomoa goli hilo kwa upande wa Chelsea na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Lakini moja ya tukio lililozua maneno mengi na mijadala kibao ni pale Salah ambaye ni raia wa Misri alipogoma kushangilia alipofunga goli hilo lililoifanya Liver kuwa mbele 1-0.
Lakini kugoma uko kwa Salah kushangilia kumezua maneno mengi ila kubwa ikifikiria kwa vile aliifunga klabu yake ya zamani ndio maana alitaka kuoyesha heshima kwa klabu hiyo ambayo hakudumu sana kutokana na kushindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Sio kweli.
Ndio sio kweli, hiyo sio sababu, ila sababu kubwa ilikuwa kwamba nchini Misri ambapo ndipo alipotokea mshambuliaji huyo kulishambuliwa na waasi wa ISIS na kufariki watu zaidi ya 300 na kwa kutokushangilia kwa Mohammed Salah kumbe alikuwa anatoa heshima kwa raia hao waliopoteza maisha.
Post a Comment
Post a Comment