Asubuhi ya leo kulikuwa na fainali ya pili ya mchezo wa basketball kwa vijana maarufu kama junior nba ambapo inafanyika tanzania kwa mara ya pili huku ikihudhuriwa na wageni rasmi Didier Mbegga ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Los Angeles Lakers inayopatikana ligi kuu ya kikapu nchini marekani maarufu kama Nba, na mgeni rasmi ambaye ni makamu wa rais wa basketball kwa Afrika ndugu Amadou Gallo Fall..
hii ni mara ya pili kwa mashindano hayo kufanyika nchini ambapo mwaka huu imeboreshwa kwa kushirikisha mashindano ya wasichana ambapo ilijumuisha klabu 30 za basketball kwa wasichana na wavulana ambapo katika fainali ya wavulana klabu ya Mzizima au Aga Khan waliibuka washindi kwa vikapu 9 dhidi ya 6 vya St. Augustine na mchezaji bora au MVP kwa upande wa wavulana aliibuka kuwa Brian Rwehumbila wakati kwa upande wa wasichana vijana wa Juhudi waliibamiza vibaya klabu ya Lord Barden kwa vikapu 12-6 huku MVP kwa upande wa wasichana akiwa ni Jesca Ngiyajie, yule aliyeshiriki katika Basketball without borders akiwa mtanzania pekee.
Post a Comment
Post a Comment