Achana na ule mzozo unaofukuta huko nchini Hispania juu ya uhitaji wa wakazi wa kitongoji cha Catalunya juu ya kutaka kujitenga, sasa kuna hii habari ambayo inaweza ikawafanya wacatalunya na wapenzi wa klabu ya Barcelona kufurahi.
Ousmane Dembele huenda akacheza dhidi ya Real Madrid katika El Clasico.
Hiyo ndio habari ya mjini kwa sasa katika vichwa vya wapenzi wa klabu ya Barcelona.
Dembele ambaye alisajiliwa akitokea Borussia Dortmund ya ujerumani alisajiliwa na Barcelona kwa dau kubwa lakini hakucheza michezo mingi na kupata majeraha mwezi septemba hali iliyomfanya atarajiwe kuwepo nje kwa kipindi cha miezi minne, yaani ilielezwa atarudi mwezi januari mwakani.
Lakini kwa taarifa zilizotoka kwa daktari aliyekuwa anamsimamia nyota zinadai kwamba huenda Dembele akawai kupona na ataweza kucheza katika mchezo wa El Classico tarehe 23 mwezi desemba mwaka huu.
Post a Comment
Post a Comment