Ni wiki nyengine ya mfululizowa michezo ya ligi kuu Uingereza, ambapo wiki hii inakuwa wiki ya 13 toka ligi hii ianze msimu huu ambapo kama ilivyo kwaida ya ligi hii huwa haikosi utamu haswa kwa mechi kubwa, mechi yenye ushindani iwe moja ama mbili lakini kila wiki kunashuhudiwa mchezo mkubwa na unaovuta hisia na macho ya watu wengi.
Siku ya leo, mchezo unaotegemewa kuvuta mashabiki na fikra za watu wengi utakuwa ule wa usiku ambapo Chelsea itasafiri kutoka jijini London mpaka kufika yalipo makao ya klabu ya Liverpool kiwanjani Anfield.
Mchezo huu ni wa muhimu kwa klabu zote kutokana na klabu hizo zinavyoshika nafasi katika msimamo wa ligi kuu, klabu ya Chelsea ikishika nafasi ya tatu wakati Liverpool aliyeko nyumbani leo anashika nafasi ya tano huku akiachwa alama 3 tu na Chelsea ambapo inamaanisha kama Liverpool atamfunga Chelsea leo basi atakuwa amepunguza tofauti ya alama na kuwa sawa na klabu hiyo wakatii kwa upande wa Chelsea itataka kushinda mchezo wa leo ili iongeze matumaini ya kulitetea taji lake.
Michezo mingine ya leo;
Crystal Palace vs Stoke city (saa 18:00)
Manchester united vs Brihton (saa 18:00)
Newcastle vs Watford (saa 18:00)
Swansea vs Bournemouth (saa 18:00)
Tottenham vs West Brom (saa 18:00)
Mchezo wa jana;
West Ham 1-1 Leicester
(Mark Albrighton-Leicester)
(Cheikhou Kouyate-West Ham)

Post a Comment
Post a Comment