Kocha wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amelalamikia upangwaji wa ratiba katika ligi kuu Uingereza.
Kuelekea katika mchezo wa klabu bingwa leo usiku ambapo Chelsea itasafiri mpaka nchi ya Azberjain kukutana klabu ya Qarabag katika mchezo wa raundi ya 5 katika kundi C.
Antonio Conte amelalamikia upangwaji wa ratiba ya ligi kuu Uingereza ambapo amedai ratiba hiyo inawafanya kutojiandaa vizuri katika michezo ya ligi kuu.
"kumekuwa na ukame kwa timu za Uingereza kufika fainali ya klabu bingwa Ulaya, hata katika hatua ya nusu fainali ambapo inatokana na wachezaji kukosa muda wa kujiweka sawa" alisema kocha Antonio Conte ambapo atahitaji kushinda mchezo wa leo usiku ili ajihakikishie kufuzu kucheza hatua ya 16 bora.
"na hii sisemi kwa timu yangu tu, ila kwa timu zote za Uingereza zinazoshiriki ligi ya mabingwa zimekuwa zikipata tabu juu ya ratiba ya ligi kuu" aliongezea Conte.
Chelsea ndio klabu ya mwisho kutokea Uingereza kucheza fainali ya klabu bingwa Ulaya ambapo ilifanya hivyo msimu wa 2011-2012.
Tuhuma hizo zilishawai kulalamikiwa pia na kocha wa Manchester united, Jose Mourinho.
Post a Comment
Post a Comment