Leo Jumapili kama wazungu wanavoitaga super sunday,jumwpili fulani ambayo inakuaga na mechi kubwa pale mjini uingereza ikitazamiwa leo Kuna Man u vs chelsea pia Man city na arsenal

Tabiri hivi ili ushinde mpunga mrefu,usiogope kabisa..

Tuanze mechi ya kwanza

TOTTENHAM VS CRYSTAL PALACE

Ni moja ya mechi ngumu sana na ni derby ya uingereza hii.Lakini ukiangalia kiufundi unaweza kuona kuwa Crystal palace hawako vizuri,wanashikiria mkia chini kabisa mwa ligi ya uingereza point zao nyingi wakizipata dhidi ya chelsea ambako wengi hawakutarajia hilo.Kikubwa zaidi timu yao bado haijakaa sawa kulinganisha na spurs ambayo ina morali ya hali ya juu baada ya kumtwanga bingwa mtetezi wa UEFA madrid 3-1 ndani ya wembley. Kwa mimi nampa chance ya ushindi spurs

TOT 2- 0 CRY

EVERTON VS WATFORD FC

Mechi nyingine kali weekend hii itakuwa kati ya hawa wawili ambapo kwa upande wa everton wengi tulitegemea watakuwa moto sana msimu huu kutokana na usajiri waliofanya.Waliweza kumsajiri Wayne Rooney,sirgusson na wengine wengi sana,Lakini mambo hayajaenda hivyo,Everton wamekuwa na matokeo mabaya sana msimu huu,huku katika mechi tatu zilizopita akifungwa zote ikiwemo 5-1 na arsenal,leicester na juzi kapigwa Europa na Lyno.Zaidi ya hapo hivi karibuni wamemfukuza kocha wao mkuu,mholanzi Koeman...kutokana na haya nafasi kubwa ya ushindi anapewa Watford ambaye yupo katika kiwango kizuri sana msimu huu na akiwa katikati ya Table pale uingereza.

EVERTON 1-2 WATFORD

MAN CITY VS ARSENAL

Mechi nyingine kubwa na inayisubiliwa na mashabiki wengi ni ya arsenal na man city,wengi wakitazamia kuwa inaweza kuwa mechi itakayoamua nani ni bingwa msimu huu.

Man city wanaongiza ligi hiyo wakiwa na point 28 baada ya michezo 10 huku arsenal akiwa na point 19 pekee.Ushindi wa man city leo inamaana itamwacha Arsenal point 12 na spurs ambaye anashika nafasi ya pili point 10.Hii inamaanisha katika mechi ya Chelsea na man u lazima mshindi apatikane,lasivyo mambo yatakuwa magumu kwa timu zote mbili huku Man u akiachwa kwa point nane na chelsea akiachwa kwa pointi 12 na vinala man city.Lakini ikitokea arsenala anshinda mchezo huu tunategemea kuona ligi ikishika kasi sana kwa sababu vinala wote watapumua.

Lakini tukirud mchezoni,Man city kwa kipindi cha hivi karibuni imekuwa moto wa kuotea mbali ulaya na uingereza,na wengi wakisema huenda ikiwa timu bora kuliko zote ambazo Guardiola amewahi kufundisha.Man city inayoongizwa na Aguero,jesus,sana na sterling,haifai kabisa.

Upande wa pili,Arsenal imekuwa timu ya kupanda na kushuka kwa miaka ya karibuni na wakiwa na matokeo mabovu wanapocheza mbali na nyumbani,kwa maana hii ni ngumu kuona kama arsenala atapata chochote kwenye mechi hii dhidi ya man city ugenini.

MAN CITU 3-1 ARSENAL

CHELSEA VS MAN U

Hapa ndipo penye kazi sasa,pande zote mbili presha ipo juu.Upande wa man u na mourinho kinachowapa presha sana ni mashabiki,mashabiki wa man u kwa siku za karibuni hawajaridhishwa na kiwango kibovu kinachooneshwa na timu yao hasa wakiwa mbali na nyumbani licha ya kushinda mechi zao takriban 2 zilizopita. swala jingine lipo kwa straika Lukako ambaye tango tarehe 30 mwezi sept hajatupia bao lolote.Ni lazima washinde mechi ya leo ili kwenda angalau karibu na man city waliopo kileleni.

Ikumbukwe kuwa Man u ni moja ya timu yenye matokeo mabaya sana Katika uwanja wa chelsea,huku msimu uliopita wakipokea kipigoa cha 4-0

Huku chelsea mambo kwao yakiwa magumu ikifuatiwa kipigo cha kati ya wiki cha 3-0 dhidi ya Roma.

Conte na chelsea msimu huu wamekuwa kivuli cha mwaka jana,chelsea mwaka jana ilikuwa moto sana ikiongozwa na muitaliano Conte.Lakini msimu huu wamekuwa na matokeo ya kusuasua sana na tetesi zikizidi kuenea kuwa huenda kibarua cha conte kikawa kwenye mashaka kufuatia mtiririko wa matokeo mabaya.

Conte anakazi ngumu sana kuhakikisha timu yake inashinda leo.

CHELSEA 1- 1 MAN U

mitaaniforum.blogspot.com

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.