Klabu ya Tottenham imefanikiwa kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 10 katika ligi kuu Uingereza. Tottenham imevunja rekodi ambayo Manchester united iliiweka miaka kumi nyuma kwa kuingiza mashabiki wengi katika mchezo mmoja ambapo klabu hiyo matajiri wa jiji la Manchester waliingiza mashabiki 76,098 katika mchezo dhidi ya Blackburn ambpo United ilishinda kwa mabao 4-1.
Lakini jioni ya leo Tottenham ikiwa Wembley uwanja ambao inautumia kama uwanja wake wa nyumbani imefanikiwa kuvunja rekodi hiyo na kuingiza jumla ya watu 80,827 katika mechi iliyoishuhudia klabu hiyo ikishinda jumla ya mabao 4-1 dhidi ya Liverpool.
Post a Comment
Post a Comment