Mchezo ulianza kwa kasi, huku Udinese wakiwa wa kwanza kupata goli la mapema, ambapo Stipe Porica aliifungia klabu hiyo goli la kuongoza mnamo dakika ya 8. Na Juventus kuwa nyuma kwa bao 1-0.
Dakika ya 14, Samir Dos Santos wa Udinese alijifunga goli na kuifanya Juventus kuanza kupumua maana ubao ulishasomeka 1-1.
Dakika 6 tena baadae yaani dakika ya 20, kiungo mjerumani Sami Khedira akaipatia klabu yake ya Juventus goli la kuongoza ambapo baadae tena kidogo winga na mshambuliaji wa klabu hiyp, Mario Mandzukic alionyeshwa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu, hali iliyofanya Juventus kutetea ushindi wakiwa pungufu. Mpaka mpira unaenda mapumziko ubao ulikuwa Udinese 1-2 Juventus.
Baada ya kipindi cha pili kuanza Udinese wakachomoa goli na ubao kusomeka Udinese 2-2 Juventus, goli lililofungwa na Danilo dakika ya 47.
Daniele Rugani wa Juventus akaifungia tena klabu yake dakika ya 52, huku Sami Khedira tena akifunga 59 na dakika ya 87 ambapo kwa magoli hayo Khedira ilimaanisha akiifunga 'hat-trick' yake ya kwanza huku kabla mpira haujaisha Miralem Pjanic wa Juventus akaongeza idadi ya magoli na mchezo kuisha matokeo yakiwa Udinese 2-6 Juventus.
Matokeo Mengine ya Serie A;
Chievo Verona 3-2 Hellas Verona
AC Milan 0-0 Genoa
Atalanta 1-0 Bologna
Benevento 0-3 Fiorentina
SPAL 2013 0-1 Sassuolo
Torino 0-1 Roma
Sampordia 5-0 Crotone
Napoli 0-0 Inter Milan
Post a Comment
Post a Comment