Unakumbuka ile timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kama Serengeti Boys? Unakumbuka ilishindwa kuvuka kikwazo cha mwisho ili kufuzu kucheza kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17, sasa kama ingefuzu huenda leo ingekuwa moja ya timu zilizomo katika hatua ya nusus fainali ya michuano hiyo amabapo inatimua vumbi huko India.

Mwafrika pekee aliyeko kwenye hatua iyo mpaka sasa ni timu ya taifa ya Mali ambapo hapo jana iliibamiza timu ya taifa ya Ghana ambaye ni mwafrika mwenzake kwa mabao 2-1.

Sasa Mali imefuzu kucheza katika ngazi ya Nusu fainali ambapo itamenyana na Hispania ambao wao wamefuzu mara baada ya kuitandika timu ya Iran kwa mabao 3-1.

Wakati Nusu fainali nyengine itakuwa ni Uingereza ambayo ilimwadhibu timu ya taifa ya Marekani mabo 4-1, ambapo Uingereza itacheza na Brazil iliyomtandika Ujerumani 2-1.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.