Ibrahim Ajib ameendelea kuwasha moto akiwa na Yanga baada ya leo Jumapili October 22, 2017 kuifungia mabao mawili kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Stand United na kuifanya Yanga ifikishe pointi 15 sawa na Simba na Mtibwa Sugar.
Simba na Mtibwa zilifikisha pointi 15 baafa ya kushinda michezo yao ya jana lakini ushindi wa Yanga leo unafanya timu tatu kufungana pointi lakini tofauti ya magoli ndio unazitofautisha katika msimamo wa ligi.
Ajib ndio anaongoza kwa ufungaji kwenye kikosi cha Yanga akiwa na magoli matano (5) aliyoyafunga kwenye mechi saba alizocheza.
Magoli ya Ibrahim Ajib
- Njombe Mji 0-1 Yanga (Ajib)
- Yanga 1-0 Ndanda (Ajib)
- Kagera Sugar 1-2 Yanga (Ajib-assist goli la kwanza likafungwa na Chirwa, yeye akafunga la pili).
- Stand United 0-4 Yanga (Ajibu amefunga magoli mawili, Pius Buswita na Obrey Chirwa wamefunga moja kila mmoja)
Anamfukuza Okwi kimyakimya
Ajibu yupo nyuma ya Okwi kwenye orodha ya wafungaji VPL, Okwi amefunga magoli nane (8), Ajib magoli matano (5) na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye magoli manne (4).
Yanga imeshinda mechi yake ya nne msimu huu sawa ikiwa imetoka sare mara tatu huku ikiwa haijapoteza mchezo sawa na matokeo ya Simba pamoja na Mtibwa Sugar huku timu zote zikiwa zimecheza mechi saba hadi sasa
- Yanga 1-1 Lipuli
- Njombe Mji 0-1 Yanga
- Majimaji 1-1Yanga
- Yanga 1-0 Ndanda
- Yanga Mtibwa 0-0 Mtibwa Sugar
- Kagera Sugar 1-2 Yanga
- Stand United 0-4 Yanga
Ushindi wa kwanza mkubwa kwa Yanga
Yanga ilikuwa haijashinda mechi kwa zaidi ya magoli mawili, huu ni ushindi wao mkubwa Tangu kuanza kwa VPL msimu huu. Walifunga goli moja mfululizo kwenye mechi zao nne za kwanza kabla ya kupata ushindi wa magoli 2-1 walipocheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliopita.
Chanzo cha habar ni shafihhauda.com
Chanzo cha habar ni shafihhauda.com
Post a Comment
Post a Comment