Liverpool iliingia katika mchezo huo ambao ulipigwa katika uwanja wa Wembley, uwanja ambao Tottenham unautumia msimu huu kama uwanja wa nyumbani na kushuhudiwa majogoo hao wakipokea kipigo kitakatifu cha mabao 4-1.
Alikuwa ni mshambuliaji machachari wa Tottenham, mwingereza Harry Kane ndie aliyefungua pazia la mabao kwa kufunga bao safi akitumia makosa ya mlinzi Lovren ambaye katika mchezo huo amevurunda sana.
Baada ya Harry Kane kufanya 'ubao' kusomeka 1-0, safari hii tena ikawa zamu ya yule Mjapan, Heung Min Son aliyefunga bao la pili kwa Tottenham akipokea pasi safi iliyotoka kwa Harry Kane aliyetumia uzembe wa Lovren kuisaidia timu yake iwe mbele kwa mabao 2-0.
Dakika kadhaa baadae, mwafrika ambaye alikuwa mchezaji bora wa wiki wa michezo ya klabu bingwa Ulaya maarufu kama Uefa Champions, Mohammed Salah akitumia udhaifu na kuonyesha umahiri wake katika kukimbi, akaisaidia Liverpool kufunga goli lake la pekee kwa siku ya leo.
Dakika kadhaa tena, Delle Alli anaifungia Tottenham goli la 3 na kufanya matokeo kuwa 3-1 na mpira kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza na kama kawaida yake, Harry Kane akatumia uzembe wa walinzi walioshindwa kuokoa mpira wa adhabu ambapo baada ya kugongana gongana basi Kane akatumia uzembe huo na kuifungia Spurs goli la 4 na kufanya mpira kuisha kwa Klopp ambaye ni kocha wa Liverpool kubamizwa 4-1.
Lakini wakati hayo yanatokea kwa Liverpool na kuifanya Tottenham kupata ushindi mkubwa uwanjani hapo, huko kwa Arsene Wenger na Arsenal yake ni furaha na kula bata tu.
Arsene Wenger ameishuhudia timu yake ikiibamiza klabu ya Everton jumla ya mabao 5-2, huku Arsenal ikipata ushindi huo ikiwa ugenini,
Hii ni furaha kwa Arsene Wenger ingawa kwa kocha wa Everton anatabiriwa kutimuliwa muda wowote kuanzia sasa, kutokana na kuwa na matokeo mabovu. Ambapo katika michezo mitano iliyopita hajapata ushindi hata mechi moja.
Ronald Koeman ambaye ni raia wa Uholanzi anaonekana kuishiwa mbinu klabuni hapo na inaelezwa muda wowote anaweza kutimuliwa baada ya kufanya vibaya licha ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa wakati wa usajili.
Magoli ya Arsenal yamefungwa na Alexis Sanchez, Lacazzette, Mesut Ozil, Nacho Monreal na AAron Ramsey wakati yale ya Everton yamefungwa na Wayne Rooney na Niasse.
Shabiki wa Everton akimdhihaki kocha wa Everto, Ronald Koeman katika mchezo dhidi ya Arsenal tarehe 22-Oktoba-2017 |
Post a Comment
Post a Comment