Leo china imezindua rasmi meli yake kubwa yakivita "manowari" yenye uzito wa tani 50,000.
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba ndege iliyotengenezwa na uchina wenyewe,inakuwa meli ya pili ya kivita nchini china baada ya ile meli ya kwanza iliyonunuliwa ukraine.
Hii ni ishara ya china kujiimarisha katika jeshi la majini.
Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.
Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.
Post a Comment
Post a Comment