Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, ameshutumu hotuba ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, akidai inaikosoa Israel kimaonevu.Netanyahu anasema Bw Kerry amekuwa akikosoa saanaa mpango wa Israel wa kupanua maakazi yao katika ardhi ya Palestinian lakini hakosoi vya kutosha uchochezi unaofanywa na Wapalestina.John Kerry ameutetea uamuzi wa nchi yake wa kuliwezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupitisha uamuzi wa wiki iliyopita, kutangaza makazi ya Wayahudi katika ardhi ya Wapalestina kuwa ni kitendo kinachokiuka sheria za kimataifa.Kerry amesema hatua hiyo ina niaya kulinda uamuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea. Amesema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.Lakini hata hivyo, Waziri mkuu waIsrael Benjamin Netanyahu ameelezea kuvunjwa moyo na hotuba hiyo, ambayo ameielezea kuwa sio sawa.Amesema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubaliuwepo wa Israel.Kwa upande wake, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makaazi mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.
By
Bbc.com/swahili
Post a Comment
Post a Comment