Hatimaye Ngamia wa Jangwani amtafuna Mmakonde.
Ni vita iliyotokea siku ya leo muda mfupi uliopita ambapo watoto wa jangwani, Yanga African wametoka kifua mbele baada ya kumtandika bila huruma mmakonde wa Ndanda FC jumla ya mabao 4-0.
Donald Ngoma ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuziona nyavu za uwanja huo wa uhuru kwa kupachika bao safi kwa kichwa. Lakini Amis Tambwe naye alicharuka na kutupia bao la pili kabla ya Donald Ngoma kuongeza tena bao la tatu. Na mpaka wanaenda mapumziko Yanga 3-0 Ndanda.
Bao la nne lilifungwa kipindi cha pili ambapo Bossou aliongeza bao la 4-0 na mpira kuisha.
Kwa matokeo hayo Yanga imebakiza pengo la point 1 kuweza kuwafikia vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara, Simba SC.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.