Timu ya Barcelona imechomoza na ushindi mwembamba mbele ya timu kigogo Sevilla baada ya Barcelona kutoka nyuma na kushinda goli 2-1.
Sevilla ndo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Vitollo lakini mchezaji bora wa dunia kwa mara 5 akachomoa goli na ubao kusomeka 1-1 kabla ya Suarez kuongeza na matokeo kuisha Barcelona akitoka kifua mbele kwa goli 2-1.
Kwa ushindi huo Barcelona inashika nafasi ya 2 ikiwa na pointi 25 huku usukani ukiongozwa na Real Madrid mwenye point 27
Post a Comment
Post a Comment