Vita kali ya mahasimu wawili inaendelea leo ambapo united inayogubikwa na mawazo baada yabkupoteza mechi nyingi ikiwemo kipigo kitakatifu walichopokea kutoka kwa chelsea jumapili hii inapokutana na man city ambayo nayo haijapata matokeo katika mechi zake Tano za mwisho katika mashindano yote ikiwemo ya kipigo cha bao 4 kutoka kwa Barca.
Utamu wa mechi ya leo upo pande mbili.Ngoja tuangalie moja moja
1.MATOKEO MABOVU YA TIMU ZOTE MBILI.
Timu zote mbili zimekuwa na matokeo mabaya katika ligi ya uingereza ambapo united inayonolewa na mreno mourinho"The special one" imekuwa ikilalamikiwa na mashabiki wake kwa kucheza mpira mbaya na usiovutia.
wasiwasi umezidi kutanda old Trafford baada ya kumapili hii united kupokea kipogo cha bao 4 kutoka kwa mahasimu wao Chelsea. Bao hizo nne zilikiwa rahisi sana kufungwa united na ndio kipigo kizito zaidi ambacho mourinho amewahi kukipokea uingereza .
Mchezaji ghali zaidi duniani Paul pogba amezidi kupokea lawama nyingi baada kuonyesha mpira mbovu tangu asajiliwe.
Kipigo hiko bado ni jinamizi kwa manchester utd ambayo katika mechi hiyo pia walimpoteza beki wao Baily.
Mshambuliaji Ibra cadabra bado anaonekana kivuli chake baada ya sasa kucheza mechi sita za ligi bila goli wala assist.haujawahi kumtokea kwa miaka 6.
Swali je,Manchester hii inaweza kuondoa gungu lake leo mbele ya city?jibu tutapata.
MANCHESTER CITY nayo ambayo inaongoza ligi kwa goli moja nayo ipo katika wakati mgumu baada ya kuanza ligi vizuri lakinisasa wamejikuta katika kiwango kibovu baada ya kucheza mechi TAno mashindano yote bila ushindi. Man city inayoongizwa na josep guardiola ilikubali kipigo cha bao 4 bila kutoka kwa wakatalunya Barcelona.
Timu hiyo ambayo inaonekana kushindwa kufunga magoli licha ya kumiliki mpira sana,inampa kocha wake wakati mgumu kwa sababu ya mfululizo wa mechi ngumu zinazofuata.
Guaediola anahitaji ushindi katika mechi hii ili kuwapa morali na ujasiri wachezaji wake.
2.VITA YA MOURINHO NA GUARDIOLA.
Wawili hawa wamekuwa na vita kali kila mara walipokutana na kufanya mechi za timu zao kuongezeka mvuto.
Wawili hawa walianza kukutana kpindi guardiola akiwa Barcelona na mou akiwa inter milan.
waliendeleza ubabe wao baada ya Mou kuhamia Real madrid na kuinogosha El classico.
Vita yao ilizidi kuwa kali baada ya mou kuhamia Chelsea na pep kwenda Bayern ambapo timu hizo zilikutana mwaka 2013 katika uefa super cup na kutoka sare ya bao 2-2.
Sasa hivi wapo tena katika Manchester Derby, ambapo mechi ya kwanza msimu huu iliyopugwa Old Trafford, pep aliinuka kidedea..
Je,nani ni nani leo?kila timu inataka ushindi ili kujiweka sawa,hakuna sare leo,hata kwa matuta lazima bngwa apatikane
@Big EviL.

Post a Comment
Post a Comment