Kiongozi wa kundi la waasi la Sudan kusini , Riek Machar, ametoa wito kuwe na vuguvugu la kivita la kuipinga serikali la nchi hiyo.
Awali bwana Machar alikuwa amerudi katika mji mkuu wa Juba kama sehemu ya utekelezwaji wa mkataba wa amani lakini akalazimika kwenda tena uhamishoni hapo Julai baada ya kuzuka mapigano yaliyowauwa mamia ya watu .
Taarifa hii ya sasa imetolewa baada ya Bwana achar kukutana na wanachama wa kundi lake huko nchi jirani ya Sudan.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa juu wa kundi lake hawamuungi mkono tena.
Mmoja wao ni Taban Deng ambae amejiunga na serikali na sasa amerithishwa wadhifa wa makamu wa rais nafasi iliyokuwa ya Bwana Machar.
Post a Comment
Post a Comment