Arsenal wakiwakaribisha basel fc emirates walitoka na ushindi wa bao 2-0 bao zote zikiwekwa kimyani na theo walcot.
Arsenal ikiwa nyumbani ilibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Basel ya nchini uswizi, magoli yote yaliwekwa kimyani na Theo Walcott.
PSG ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.
Besiktas imeenda sare ya 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv. Huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.
Borussia Moenchengladbach nayo ikiwa nyumabi imekubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Barcelona. Na mchezo wa kushangaza wa funga nikufunge ulikuwa kati ya Celtic na Manchester City, ambazo zilienda sare ya 3-3.
Atletico Madrid nayo ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Na FC Rostov ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven
Post a Comment
Post a Comment