Umoja wa Mataifa umezindua rasmi kampeni  ya kukusanya kiasi cha dola za Marekani, milioni 952, kwa lengo la kuisaidia nchi ya Sudan kukabiliana na janga la kibinadamu.

Mpango huu ambao ulicheleweshwa ili kuzungumzia mahitaji ya kibinadamu kwa watu zaidi ya milioni 4 na laki 6, wakiwemo maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wamekimbilia Sudan, wakikimbia machafuko na uhaba wa chakula kwenye nchi yao.

"Wanawake, wanaume, wakimbizi na wakimbizi wa ndani, wanatutaka sisi kuongeza juhudi kutoa msaada kwao," aliripoti Naeema Al-Gasseer, mratibu wa misaada ya kibinadamu kwa nchi ya Sudan.

Al-Gasseer, ameongeza kuwa fedha zitakazopatikana, zitatumiwa kufikia malengo ya mahitaji ya kinadamu kwa watu walionaswa kwenye machafuko jimboni Darfur.

Machafuko kwenye jimbo la Darfur yalianza mwaka 2003 wakati jamii ya makabila madogo kwenye eneo hilo, walipoanza kushika silaha kumpinga Rais Omar al-Bashir, wanayemtuhumu kupendelea waarabu.

Kufuatia uasi huo, Rais Bashir na Serikali yake walianzisha vita kuwakabili watu waliokuwa wanaipinga Serikali yake, ambapo zaidi ya watu laki 3 waliuawa kutokana na vita hivyo, huku umoja wa Mataifa ukisema kuwa zaidi ya watu wengine milioni 2 na laki 5 wakikimbia nyumba zao.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.